Kaimu Katibu Mkuu Wa TFF Salum Madadi

Kamati Ya Uchaguzi Ya TFF Yawapiga Chini Wajumbe Wenye Matatizo.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Salum Madadi

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Salum Madadi

Kamati ya utendaji ya TFF imekutana kwa dharura na kufanya marekebisho kwenye kamati zake mbalimbali lakini marekebisho kwenye kamati ya uchaguzi wa TFF ndio ilikuwa ikisubiriwa kwa shauku kubwa na kila mpenda soka la Tanzania.

Uamuzi uliofikiwa na kamati ya utendaji ya TFF ni kuwaondoa baadhi ya wajumbe wa kamati ya uchaguzi na kumuacha mmoja tu Revocatus Kuuli ambaye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya awali kabla ya kufanyiwa marekebisho na ataendelea kuwa mwenyekiti kwenye kamati mpya iliyoteuliwa.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Salum Madadi amewataja wajumbe walioteuliwa kuunda kamati mpya mpya cha uchaguzi vilevile ametaja sababu zilizozingatiwa katika kuwaondoa wajumbe wa kamati ya awali.

Baada ya Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukaa na kufikia uamuzi wa kuwaondoa katika kamati ya uchaguzi wajumbe wanne na kuweka wapya, yafuatayo ni majina ya walioondolewa na wapya.

Wajumbe walioondolewa katika kamati ya uchaguzi ni wafuatao.
1. Juma Lalika
2. Dominated Madeli
3. Jeremiah Wambura
4. Omary Hamidu

Wafuatao ndiyo wajumbe wapya watakaoungana na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Wakili Revocatus Kuuli.
1. Mohammed Mchengela
2. Wakili Malangwe Ally
3. Wakili Kilomoni Kabamba
4. Wakili Deus Kalua

Leave a Reply