Zanu Pf Mugabe

Mugabe Atakiwa Kujiuzulu.

Vyama vya upinzani nchini Zimbabwe vimerejelea wito wao wa kutaka Rais Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 93 ajiuzulu, na kumlaumu kwa kuiongoza nchi kutoka hospitalini kufuatia madai kuwa alisafiri kuenda Singapore kwa matibabu.

“yeye bado si kijana mdogo, njia hii anajiadhibu sio nzuri kwa afya yake ya kimwili na kiakili. Mugabe ni lazima aondoke na aiache Zimbabwe kusonga mbele chini ya uongozi mpya.”

Wakati huohuo chama cha Zanu-PF kimemteua bwana Mugabe kuwania urais mwaka ujao licha ya kuonekana kutokuwa na afya nzuri na amekuwa madarakani tangu mwaka 1980.

Leave a Reply