TELEMMGLPICT000136969995 Trans NvBQzQNjv4BqpVlberWd9EgFPZtcLiMQfyf2A9a6I9YchsjMeADBa08

Gari Lawagonga Wanajeshi Wa Ufaransa Mjini Paris 6 Wajeruhiwa.

Gari moja limegonga kundi la wanajeshi mjini Paris, Ufaransa na kuwajeruhi sita na  wawili kuumia vibaya.Oparesheni ya dharura inaendelea kutafuta gari hilo na dereva aliyetekeleza kitendo hicho katika mtaa wa Levallois-Perret.

Meya wa eneo hilo Patrick Balkany, amesema hana shaka kuwa kitendo hicho kilikuwa ni cha makusudi.

Ufaransa imekuwa chini ya hali ya tahadhari tangu mwezi Novemba mwaka 2015.Tangu wakati huo zaidi ya watu 230 wameuawa kwenye mfululizo wa mashambulizi ya kigaidi.

Hayo ni pamoja na mashambulizi dhidi ya vikosi vilivyojihami ambavyo  vimetapakaa sehemu tofauti mjini humo.

Shambulizi hilo lilitokea karibu na ukumbi wa mji ulio mtaa wa Levallois-Perret.

Leave a Reply