CBE 5

Mkuu wa Mkoa Wa Dar es salaam Paul Makonda Ametoa Wito Kwa Wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul Makonda ametoa wito kwa wananchi, makampuni, taasisi za dini na mashirika kusaidia watu wenye ulemavu zaidi ya 650 ambao wameongezeka katika zoezi la upimaji wananchi waliopata ajali ya miguu kwa ajili ya  kupatiwa miguu bandia.

Ongezeko hilo linatokana na baadhi ya wananchi wenye ulemavu wa miguu kutoka katika mikoa mbali mbali nchini badala ya wale 200 wa awali ambao walipatiwa miguu bandia na kampuni ya kutengeneza Nondo ya Kamal steel ya jijini dsm,ambapo taasisi ya mifupa moi pamoja na Hospitali ya CCBRT imejitolea kusaidia zoezi hilo.

Baadhi ya wadau wameamua kuunga Mkono zoezi hilo la kuchangia kwa njia moja ama nyingine na kutoa wito kwa wananchi wengine watakaoguswa kujitokeza katika katika kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa dsm katika kusaidia wananchi masikini wasiokuwa na Uwezo.

Leave a Reply