1fa678d65613665fb6d57c1649e1f3e6

Prof Jay: Diamond Ni Mfano Wa Kuigwa.

Baada ya msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kukiri wazi kuwa mtoto wa Mwanamitindo, Hamisa Mobeto kuwa ni wa kwake. Hatimae Mbunge wa jimbo la Mikumi, Joseph Haule a.k.a Professor Jay amempongeza mkali huyo kwa kitendo hicho.

Professor Jay amesema Diamond Platnumz kwa kitendo hicho amekuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii kwani kuna watu wengi wanapitia changamoto kama hizo.

Ukweli humuweka Mtu huru kweli kweli, Big up mdogo wangu @diamondplatnumz Umekuwa Mfano bora sana,ameandika Professor Jay kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Leave a Reply