Mafuta(4)

Mafuta Yakamatwa Tanga Toka Malaysia.

Maafisa forodha kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoani Tanga wamefanikiwa kukamata shehena ya mafuta ya kupikia kutoka nchini Malaysia yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 47.3 yaliyokuwa hayajalipiwa ushuru kisha kutaifisha magari mawili aina ya Fusso yaliyokuwa yamebeba bidhaa hiyo iliyoingizwa nchini kinyume cha sheria.

Akizungumza na ITV kuhusu zoezi hilo,meneja forodha mkoa wa Tanga jumbe magoti amesema mafuta hayo yanayojulikana kwa jina la ”SHAKIRA” yamekamatwa katika bandari bubu iliyopo eneo la Mtimbwani wilayani Mkinga baada ya wafanyabiashara husika kubaini kuwa maeneo waliyokuwa wakipitisha bidhaa hizo likiwemo la kigombe hivi sasa limedhibitiwa.

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoani Tanga Benedict Wakulyamba amesema hivi sasa wameandaa mpango wa kuhakikisha kuwa wanawakamata wamiliki wa magari husika badala ya madereva wanaodai kuwa hawamfahamu mwenye mali ili kukomesha ukwepaji wa ushuru ambao ni sawa na shauri la uhujumu uchumi.

Katika hatua nyingine kamanda Wakulyamba amesema watu wawili wenye jinsi ya kiume wamekutwa wamekufa katika nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Bomai wakiwa wamefungwa kamba za miguuni na mikononi huku wakiwa na michubuko mwilini ambao inadaiwa kuwa ni wafanyabiashara kutoka jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply