Syria

Shambulio La Kemikali Nchini Syria: Wachunguzi Waruhusiwa Kuzuru Douma

Wachunguzi wa silaha za kemikali nchini Syria wataruhusiwa kuzuru katika eneo linalodaiwa kushambuliwa na silaha za sumu siku ya Jumatano, kulingana na Urusi.

Kundi hilo la kimataifa limekuwa nchini humo tangu siku ya Jumamosi lakini halijaruhusiwa kuingia Douma.

Shambulio hilo la siku ya Aprili 7 lilivutia shambulio dhidi ya serikali ya Syria lililotekelezwa kwa pamoja na Marekani, Uingereza na Ufaransa wiki moja baadaye.

Syria na mshirika wake Urusi wamekana shambulio lolote la kemikali huku Urusi ikitaja madai hayo kama ‘yaliopangwa’.

Mapema siku ya Jumanne , chombo cha habari cha Syria kilisema kuwa ulinzi wa angani wa taifa hilo ulikabiliana na shambulio la makombora juu ya nga ya magharibi mwa mji wa Homs.

Makombora hayo yalilenga kambi za wanahewa wa Shayrat lakini haikusema ni nani aliyetekeleza mashambulio hayo.

Leave a Reply