Nyungwe Canopy Walk

Uvumi Kuhusu Ukosefu Wa Usalama Chini Rwanda Watupiliwa Mbali.

Mamlaka nchini Rwanda zimetupilia mbali uvumi kuhusu kuwepo ukosefu wa usalama maeneo yanayozunguka msitu wa Nyungwe, ambapo kundi jipya la waasi wa MRCD linalodai kuwa linataka kuangusha uongozi wa Rais Paul Kageme linasemekana kuwa na ngome yake.

Akiongea na wenyeji wa wilaya wa Nyaruguru, inspekta mkuu wa polisi Emmanuel Gasana alisema kuwa licha ya majambazi wachache kuvuka na kuingia Rwanda na kuwapora watu eneo moja la Nyaruguru hali hiyo ilikuwa imeshughulikiwa vilivyo na vikosi vya usalama na majambazi hao kukimbilia eneo walilotoka.

Leave a Reply