Kanye West

KANYE WEST KATUA AFRIKA KUMALIZIA ALBAMU YAKE

Rapper na producer wa muziki kutoka Marekani, Kanye Omari West amesema kuwa hakuweza kuiachia albumu yake ya 9  inayokwenda kwa jina la “Yandhi” usiku wa Jumamosi iliyopita hadi atakapo zuru ardhi ya bara la Afrika.

Kanye ambaye juzi alibadilisha jina lake nakujiita YE aliiambia tovuti ya TMZ jana siku ya Jumatatu kuwa anahisi anahitaji kwenda Afrika huku akiamini kuwa bado hajamaliza kurikodi.

“Nimehamasika na ninahisi nahitaji kwenda Afrika ili nipate mwamko mpya. “Nitakapozuru Afrika na kugusa ardhi ya bara la Afrika ndipo nitakapoikamilisha,” amesema

Msanii huyo amesema kuwa anatarajia kutua Afrika wiki chache zijazo ili kukamilisha ‘project’ yake huku lengo kuu likiwa ni pamoja na kupata mwamko mpya.

West ameongeza kuwa albamu hiyo imesogezwa mbele hadi Novemba 23 ambayo itakuwa siku ya Ijumaa hii ni baada ya uongozi wake kuhitaji muda zaidi.

Leave a Reply