103705219 Mkhiindex Getty

KIONGOZI WA ARSENAL KUSHINDWA KUSAFIRI AZERBAIJAN MECHI YA LIGI YA ULAYA.

Kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan hataweza kuwachezea katika mechi yaligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League, dhidi ya klabu ya Qarabag.

Hii ni kutokana na uhasama wa kisiasa ambao umekuwa ukiendelea kati ya taifa lake la Armenia na Azerbaijan.

Mkhitaryan, 29, hakuweza kusafiri pamoja na wachezaji wenzake kwenda mji mkuu wa taifa hilo, Baku, Jumatano kwa ajili ya mechi hiyo ya Alhamisi.

Hakuna uhusiano wowote wa kidiplomasia kati ya Armenia na Azerbaijan kutokana na mzozo wa muda mrefu kuhusu eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh.

Leave a Reply