Korosho 3 1024×767

KOROSHO ZA MAGENDO ZANASWA MTWARA

Ikiwa ni siku moja tu baada ya Rais John Pombe Magufuli kutangaza kuwa Serikali itanunua korosho kwa bei ya Tshs 3,300/= kwa kilo moja na zoezi kusimamia Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) huku akipiga Marufuku Uingizwaji wa korosho kimagendo kutoka nje ya Tanzania mapya yameibuka Mtwara.

Mkuu wa Wilaya ya Newala mkoani Mtwara, Aziza Mangosongo amemkamata mtu mmoja akiingiza Korosho za magendo kiasi cha magunia zaidi 90 yenye kilo zaidi 100 kila moja kutoka nchini Msumbiji katika maeneo ya mpakani akivusha korosho hizo jana Novemba 14, 2018.

DC Aziza akiwa na Wajumbe Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Newala alimkatama mtuhumiwa huyo wakati wa Operation Maalumu inayoendelea wilayani humo kudhibiti uingizwaji wa Korosho hizo za magendo kama Rais alivyoagiza.

Mhe Aziza amewataka wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Serikali kuendelea kufichua vitendo vichafu kutaka kuihujumu nchi na ukiukwaji wa sheria.

Leave a Reply