77a29f0849

WAANDISHI WA HABARI UGANDA WAISHTAKI MAMLAKA YA MAWASILIANO ‘UCC’

Waandishi habari katika kampuni 13 za vyombo vya habari Uganda, walioagizwa wasitishwe kazi na mamlaka ya mawasiliano nchini, wanawasilisha kesi kesho Jumatano kupinga agizo hilo.

Mamlaka ya mawasiliano Uganda (UCC) iliziambia kampuni hizo zichukue hatua dhidi ya baadhi ya wasimamizi, na wakuu wa vipindi kufuatia tuhuma kwamba wamekiuka maadili ya utangazaji katika kuangazia matukio yanayomhusu Bobi Wine, mwanasiasa wa upinzani na mkosoaji wa serikali.

Kesi hiyo inaotazamwa kama mtihani mkubwa kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini Uganda.

Waandishi kadhaa wa habari wamepewa majukumu mbadala ya muda kwa mwezi ila hawakusimamishwa kazi, kukisubiriwa matokeo ya kesi hiyo.

Katika mkutano wiki iliyopita na wamiliki vyombo vya habari, mkurugenzi mtendaji wa tume hiyo ya mawasiliano, Godfrey Mutabazi, aliridhia kwamba waandishi waliotuhumiwa wakae kando wakati wa uchunguzi kubaini iwapo “tabia ya mtu” “iliambatana na kilichokuwa kinatangazwa hewani.”

Muungano wa waandishi habari Uganda (UJA) unataka mahakama iizuie mamlaka hiyo ya mawasiliano dhidi ya kuagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa waandishi habari hao.

Kadhalika unataka mahakama itoe agizo la kuizuia UCC kupata kanda ya taarifa ya habari iliyotangazwa Aprili 29.

Jumatano, Mei Mosi 2019, mamlaka nchini Uganda zilitoa madai ambayo bila shaka inaangazia ni kwa namna gani uhuru wa vyombo vya habari nchini humo na ukanda mzima wa Afrika Mashariki ulivyo mashakani.

Amri iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano ya Uganda (UCC) imeagiza vituo 13 vya radio na Televisheni kuwafuta kazi ndani ya siku tatu waandishi waandamizi 39 kwa kutoa habari zilioitwa kuwa ni za ”upotoshaji’ na kuchochea ghasia kwa kutangaza taarifa zilizo na “ujumbe wenye hisia kali”.

Tume hiyo inasema kuwa vyombo hivyo vya habari vilikiuka kanuni ya kifungu cha 31 ibara ya 4 ya sheria ya mawasiliano ya Uganda ya mwaka 2013

Leave a Reply